Thursday 6 April 2017

Mbowe atakiwa kuripoti kamati ya maadili ya Bunge



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amemtaka Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani bungeni ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro Freeman Mbowe kuripoti kamati ya maadili ya bunge

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai amemtaka Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani bungeni ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro Freeman Mbowe kuripoti kamati ya maadili ya bunge ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Spika Ndugai ameyasema hayo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni ambapo amesema Mbowe anatakiwa kuripoti mbele ya kamati ya maadili ya bunge kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya lugha mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa wabunge wa bunge la Afrika mashariki uliofanyika April 4 bungeni mjini Dodoma.

Sambamba na hilo spika pia amesema zoezi la kuwaita viongozi kwenye kamati ya maadili litakua endelevu wakiwemo wabunge ili kulinda heshima ya viongozi wote kwa upande wa bunge na serikal

No comments:
Write comments