Sunday 9 April 2017

Utekelezaji Ilani ya Uchaguzi,CCM yahimiza ushirikiano mashina na matawi


Chama cha mapinduzi CCM kimewataka viongozi wake kuanzia ngazi ya shina, matawi mpaka taifa kuhakikisha wanatoa ushirikianano kwa serikali katika kutekeleza ilani ya chama hicho kwa kufanikisha mikakati Serikali katika kuwatumikia watanzania ikiwa ni pamoja na kuleta maendeleo kwa taifa kiujumla.

Hayo yamesemwa na naibu katibu mkuu wa chama cha mapinduzi bara Bw. RODRICK MPOGOLO alipokuwa akizungumza na kikao cha Sekretariet mkoa wa Mara na halmashauri kuu ccm wilaya ya Musoma mjini na Butiama katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa CCM mkoani mara uliopo mjini Musoma.

Naibu katibu mkuu huyo Amesema ili kukiimarisha chama hicho na kuijenga tanzania mpya ni wazi kuwa ipo haja kwa wanaccm CHINI kote kuhakikisha wanakuwa kitu kimoja kwa kumaliza tofauti zao ili kuliletea taifa maendeleo.

Wakati chama hicho kikitaraji kufanya uchaguzi kwa viongozi wapya wa mikoa na wilaya kote nchini naibu katibu mkuu akatoa onyo kali kwa mgombea na wapiga debe kutojihusisha na utoaji na upokeaji rushwa.

No comments:
Write comments