Wabunge hao wakiongozwa na mbunge wa Nzega Mjini, Husein Bashe (CCM), amesema kuwa kwa muda sasa amekuwa akipokea ujumbe wenye vitisho, huku akiongeza kuwa amepata taarifa kutoka kwamba muda wowote anaweza kuuawa.
Aidha, Bashe ameongeza kuwa kuna orodha ya wabunge wengine kumi ambao wanawindwa na kikundi hicho ambapo tayari wameshatahadharishwa.
Naye mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema) amesema kuwa katika bunge hilo hakuna aliye salama kwani lolote linaweza kutokea kwa mtu yeyote, hivyo amesema hakuna haja ya kutojadiliwa jambo hilo bungeni.
Hata hivyo, Naibu Spika amesema kuwa jambo la dharula linaloweza kujadiliwa ni lile lenye maslahi kwa umma na iwapo utatuzi wake unategemea zaidi utekelezaji wa kawaida wa sheria.
No comments:
Write comments