Rais Donald Trump na Rais Xi jinping
Rais wa Marekani, Donald Trump amemsifu rais wa China, Xi jinping kwa kuiunga mkono Marekani na jitihada zake za kupambana na mpango wa Nuklia wa Korea kaskazini.
Trump amesema kupata ushirikiano huo wa kupambana na Pyongyang ilikuwa muhimu kuliko kuishinikiza Beijing kuhusu masuala ya biashara.
Rais Donald Trump amesema aliamini kuwa Rais Xi alikuwa akiishinikiza Korea kaskazini, ikitaka, mazungumzo yafanyike kuhusu silaha za Nuklia za Kim Jong Un
''Rais wa China, Rais Xi, ninaamini amekuwa akimshinikiza pia.lakini mpaka sasa, pengine hakuna kilichotokea na pengine kimetokea. Hili lilikua kombora dogo, halikuwa kombora kubwa, halikuwa jaribio la Nuklia, ambalo alitegemewa kulitekeleza siku tatu zilizopita, tutaona nini kitakachoendelea''
Trump ametahadharisha kuwa mgogoro wowote wa kijeshi na Korea kaskazini unaweza kugharimu maisha ya mamilioni ya watu.
Aliyasema hayo kwenye mahojiano na chombo cha habari cha CBS cha Marekani ambapo alizungumzia hali ya mvutano iliopo kati ya nchi yake na Korea kaskazini.
Trump amesema rais wa Korea kkaskazini , Kim Jong Un ameendelea kubaki kwenye utawala wa Korea kaskazini, ingawa wamekuwepo wale ambao wangeweza kumpinga
''alikuwa kijana mdogo wa miaka 26 au 27 hivi, alipochukua mamlaka kutoka kwa baba yake, baba yake alipofariki. Ni wazi kuwa anakabiliana na watu wenye nguvu zao, majenerali na wengine.Katika umri huo mdogo, aliweza kuchukua madaraka.Watu wengi, nina uhakika, walijaribu kuyachukua madaraka hayo, pengine, mjomba wake au mtu mwingine yeyote.hivyo ni wazi kuwa ni kijana mwerevu, lakini tuko kwenye hali ambayo hatuwezi kuifumbia macho, hatuwezi kuruhusu kilichokuwa kikiendelea kwa miaka mingi kiendelee''
Siku ya jumapili,Kiongozi huyo wa Marekani alizungumza na Mawaziri wakuu wa Thailand na Singapore kujadili namna ya kuishinikiza Serikali ya rais wa Korea kaskazini, Kim Jong
No comments:
Write comments