Mkuu
wa Arusha Mrisho Gambo amesema serikali itaendelea kuwathibiti watu
wote watakaotaka kuingiza siasa kwenye majanga mbalimbali hasa la vifo
vya wanafunzi wa Lucky Vicent na kuwataka watu kufuata utaratibu na
maelekezo yanayotolewa na serikali.
Mkuu
wa mkoa huyo alisema hayo juzi wakati anapokea misaada inayoendelea
kutolewa na wadau mbalimbali na kuwataka wananchi na taasisi
zinazoendelea kutoa rambirambi kwa familia za wanafunzi waliofariki
kufuata taratibu zilizowekwa ili kuepusha migongano isiyo ya lazima.
Mbali
na hilo Gambo alisisitiza kuwa serikali itaendelea kuwadhibiti wote
watakaotaka kuingiza siasa kwenye majanga likiwemo la vifo vya wanafunzi
na amesisitiza umuhimu wa kila mmoja kufuata sheria, taratibu na
maelekezo yanayotolewa na serikali.
No comments:
Write comments