Meya
wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro amesema kuwa ataelekeza fedha zote za
rambirambi kwa wafiwa badala ya kuzipeleka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Mrisho Gambo.
Aidha
amehoji ni kwanini fedha za rambirambi zilizochangwa kwaajili ya msiba
wa wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja kuchotwa Sh.milioni 1.5
kupelekwa kama rambirambi katika msiba wa bwana na bibi harusi
waliosombwa na maji Kata ya Sambasha iliyopo Wilayani Arumeru kama pole.
Meya,
Lazaro aliyasema hayo leo Jijini Arusha wakati alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuachiliwa na Jeshi la Polisi jana majira ya saa 12:30 asubuhi kisha kwenda ofisi ya Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Kaskazini.
Amesema
fedha hizo za rambirambi zitakazochangwa na watu mbalimbali kisha
kuletwa kwake kama Meya wa Jiji la Arusha, atazielekeza kwa wafiwa moja
kwa moja badala ya kwa RC Gambo kwani RC huyo anaonekana kutumia fedha
hizo kwa malengo mengine na kumtuhumu kuwa anachukua fedha zinazochangwa
na kupeleka kwenye misiba ambayo ilitokea kipindi cha nyuma kama
rambirambi.
Amesema
wafiwa wanahoji ni kwanini fedha zilizobaki zilazimishwe kujenga jengo
la Wagonjwa Mahututi (ICU) Sh,milioni 56 huku akijua kabisa fedha hizo
zimechangwa kwaajili ya rambirambi kwa wafiwa.
“Yani
hili jambo ni la ajabu sana nimefika shuleni kutoa rambirambi na si
mimi bali nimewasindikiza umoja wa shule binafsi na nikaomba viongozi wa
dini wafanye sala kwaajili ya kuanza kutoa fedha hizo lakini cha ajabu
nakamatwa kwa kosa gani ,na mimi nasema sitaelekeza fedha kwa RC Gambo
ambazo ni za rambirambi bali zikija kupitia ofisi yangu nitazielekeza
kwa wafiwa ambao wapo kwenye kila Kata,” alisema na kuongeza;
"Mimi
ni Diwani wa Sokoni One, Wazazi waliofiwa wako 6 kwenye kata yangu,
Diwani wa Olasiti ana familia 11 zilizofiwa… na Diwani mwingine Credo
ana familia 6 zilizopoteza watoto, kwahiyo nikawaambia Madiwani wangu
wahakikishe hizo familia zinakuwepo pale shuleni.
"Moja
ya vitu Wadau hao walitaka kuwe na maombi na nilimuandaa Padri wa
Kanisa Katoliki, Mchungaji wa KKKT na kiongozi wa BAKWATA kutoka
Olasiti, kabla ya zoezi la kukabidhi rambirambi mkononi kwa Wafiwa
Polisi walivamia.
"Maswali
tulikua tunahojiwa ni kwanini fedha hizi hatujazipitisha kwa mkuu wa
mkoa? nataka Watanzania wajue kwamba hakuna Kiongozi wa Serikali
aliyefariki, walifiwa Wananchi wa kata zetu… mimi Meya wa jiji nimefiwa
na Wananchi wangu"
Naye
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya
Kaskazini, Amani Golugwa alisema tukio lile ni tukio la aibu na wakati
Fulani walimshauri RC Gambo awe mtu mzima akiendelea na mambo haya
hatafika mbali.
Awali jana(yani juz)i Mei 19, 2017, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wakati akipokea
msaada uliochangwa na wananchi kupitia tovuti ya wezesha sasa ambapo
alipokea msaada wa takriban shilingi milioni 4 alisisitiza kuwa
wanasiasa waache kutumia msiba kwa kuingiza siasa kwani hakuna fedha
yoyote ile iliyoliwa na pia wapo katika harakati za kuwatumia fedha
wazazi pamoja na timu ya wataalam wa afya walioongozana na watoto wa
Lucky Vicent ambao ni majeruhi wanaotibiwa nchini Marekani kama fedha za
kujikimu na kiasi kilichobaki hadi sasa ni zaidi ya Sh, milioni 56
ambazo kunakamati ndogo ya wazazi iliyoteuliwa ambao wataamua zitumikaje
kwaajili ya kumbukumbu za watoto hao.
No comments:
Write comments