BAADA ya Yanga Kukiri kuwa wameshindwa kufikia maamuzi ya kumbakiza kiungo wa kimataifa wa rwanda Haruna Niyonzima, sasa kiungo wa mbeya City Raphael Daudi Loth ndio anayetajwa kuwa Mbadala wa Niyonzima Yanga.
Yanga walikuwa katika mipango ya kumnasa Raphael muda mrefu lakini walikuwa wanasubiri muafaka wa kiungo wao Haruna Niyonzima, kama Anabaki au anaondoka ila baada ya Mchongo wa kumbakiza kugonga Mwamba majeshi yote rasmi yakahamishwa kwa Raphael Daudi.
Raphael ambaye kwa misimu mitatu amekuwa injini ya Mbeya City, anatajwa kuwa mtu sahihi wa kuziba pengo la Niyonzima katika nafasi ya kiungo wa kati.
Kinachosubiliwa Kwa sasa Raphael kusaini Yanga ni Kaka yake pamoja na wakili wake ambao Wapo mbeya watakuja Dar muda wowote kukamilisha usajili huo, akidhibitisha hilo Raphael Daud alisema
“Nimekubaliana na Yanga kila kitu na tumefikia mwafaka wa kusaini mkataba nao kinachosubiliwa ni Kaka yangu na wakili wangu ili kusaini mkataba huo”
Habari kutoka Yanga, Kaka yake Raphael Daudi pamoja na wakili wake watamalizana na Yanga wiki ijayo kwa kuwa kwa sasa Raphael Daud ameondoka na timu ya taifa ya Tanzania kwenda Afrika kusini kwenye michuano ya Cosafa itakayoanza Jumapili June 25
No comments:
Write comments