Akizungumza leo kwa simu kutoka Zambia, Lwandamina amesema kwamba mashindano hayo yamekuja wakati tayari ratiba ya yeye kwenda mapumzikoni imekwishapangwa.
Na Mzambia huyo aliyeiwezesha Yanga kutetea taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, amesema kikosi kitashiriki michuano ya SportPesa chini ya kocha Msaidizi, Juma Mwambusi.
Hata hivyo, Lwandamina amesema anafahamu wachezaji wake wengi wa kikosi cha kwanza wapo na timu zao za taifa, hivyo hawatapatikana kwenye michuano hiyo.
Amewataja wachezaji hao ni kipa Benno Kakolanya, mabeki Hassan Kessy, Mwinyi Mngwali na kiungo Simon Msuva waliopo na kikosi cha Tanzania kilichoweka kambi Misri, kujiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Lesotho. Juni 10 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wengine ni Amissi Tambwe aliyekwenda Burundi, Haruna Niyonzima aliyekwenda Rwanda, Thabani Kamusoko aliyekwenda Zimbabwe wote kujiunga na timu zao za taifa kwa mechi za kufuzu AFCON 2019.
“Na bado timu imemaliza msimu ina majeruhi, ambao sidhani kama watakuwa wapo tayari kucheza kama Donald Ngoma,”amesema.
Lwandamina amesema ayakuwa nyumbani Zambia kwa mapumziko ya wiki mbili, kabla ya kurejea Dar es Salaam kuanza maandalizi ya msimu mpya.
No comments:
Write comments