Saturday 3 June 2017

MADRIN WAVUNJA REKODI WATETEA UBINGWA WAO WAUTAFUNA MFUPA ULIOWASHINDA BARCA

Real Madrid  wamekuwa Timu ya Kwanza kumudu kutetea Ubingwa wao baada ya kuitandika Juventus Bao 4-1 kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI iliyochezwa huko Millenium Stadium, Jijini Cardiff, Wales.
Hii ni mara ya 12 kwa Real Madrid kuwa Mabingwa wa Ulaya.

Juventus, ambao wameshinda Fainali zao 2 tu kati ya 8 walizotinga, sasa wamefungwa katika fainali 5 mfululizo walizocheza ambazo ni za Miaka ya 1997, 1998, 2003, 2015 na hii ya 2017.

Tangu AC Milan wafanikiwe kutetea Ubingwa wa Ulaya Miaka ya 1989 na 1990, wakati huo Kombe hili likiitwa, EUROPAEN CUP, hakuna Timu iliyowahi kutetea Taji hili la UEFA CHAMPIONZ LIGI hadi msimu huu ambapo Real Madrid wameweka Historia kwa kuwa timu ya kwanza kutetea taji hili.

CR7 ambaye pia ni Mchezaji Bora wa Duniani amefikisha Maba 105 ya UCL na Msimu huu ndie Mfungaji Bora wa Mashindano haya akiwa na mabao 12 akimpiku Lionel Messi wa Barcelona aliefunga Bao 11.

kwa upande wa Karim Benzema amefikia rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid na timu ya Taifa ya Ufaransa Raymond Kopa ambaye naye alichukua vikombe viwili vya ligi na vitatu vya michuano ya ulaya,Benzema na Kopa wote ni wafaransa ambao asili yao ni Afrika na wote wamevichezea vilabu viwili tu Benzema akiichezea Lyon na Madrid anayoichezea hadi hivi sasa huku Raymond akikipiga na Real Madrid pamoja na
Stade de Reims

Madrid walitangulia kujipatia goli kupitia kwa Cristiano Ronaldo dk 20 kabla ya
Mario Mandzukic 27 kuwasawazishia juve magoli mengine ya madrid yalifungwa na
Carlos Casemiro dk 61,kisha Cristiano Ronaldo akarudi nyavuni dk 64 na super sub
Marco Asensio akagongelea msumari wa mwisho dk 90

Juve walimaliza Fainali wakiwa pungufu  baada ya Juan Cuadrado, alieingizwa Uwanjani Kipindi cha Pili, kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kufuatia Kadi mbili za manjano .
HABARI NA AMANI KAVISHE (KING LUDO)

No comments:
Write comments