IKIWA imepita miezi michache tangu ajiapize kuwa hatakuja kujichora
tattoo ya mwanaume yeyote atakayekuwa naye katika uhusiano, muuza sura
kwenye video mbalimbali za wasanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy
Money’ ameumbuka baada kunaswa akiwa amejichora jina la mwandani wake,
Mourad Alpha ‘Moj’.
Mwanadada huyo ambaye mara kwa mara amekuwa akiingia kwenye mgogoro na
Moj kwa madai kuwa amekuwa akimpiga bila sababu za msingi hivyo anatumia
nguvu kubwa kuachana naye lakini anashindwa, amejikuta akiumbuka kwa
kujichora tattoo ya jina lake. Alipobanwa baada ya kunaswa na tattoo
hizo, Gigy alisema; “Haa unaniuliza, sijui hata nikujibu nini? Nguvu ya
mapenzi ndiyo imenisababisha kufanya hivi, migogoro ni kawaida katika
mapenzi na kupigwa kila wakati nimeshazoea
No comments:
Write comments