Kiungo huyo machachari ameacha na Yanga baada ya kucheza misimu sita mfululizo na amesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya zaidi ya milioni 100 za Kitanzania.
Habari kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa, Haruna atapewa jezi hiyo iliyokuwa ikitumiwa na Mwinyi Kazimoto.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kazimoto hayupo kwenye mipango ya mwalimu kwa msimu ujao baada ya mkataba wake kumalizika.
Haruna ambae ni kipenzi cha wana Yanga, atatumbulishwa rasmi na timu yake mpya katika sherehe za Simba Day Agosti, mwaka huu.
USIKOSE HABARI HII BONYEZA HAPA KUONA KWA UNDANI KICHUYA AUNGURUMA
No comments:
Write comments