Thursday 29 June 2017

SIMBA WAPATA PIGO

Rais wa Simba Evans Aveva na Godfrey Nyange wamepelekwa Rumande baada ya kukabiliwa na mashitaka matano ikiwemo ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana.
Washitakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kutakatisha fedha ambayo ni dola za Marekani 300,000 walizozipata kwa kughushi nyaraka kuonesha kwamba Club ya Simba imelipa deni la fedha hiyo kwa Aveva.
Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alisema mashitaka hayana dhamana hivyo aliahirisha hadi Julai 13 mwaka huu kujua hatua ya upelelezi umefikia wapi.
MAKOSA 5 YALIYOTAJWA KWENYE KESI
Makosa 5 yanayowakabili Rais wa Simba Aveva na makamu wake Kaburu
1. Kughushi 
Aveva alighushi nyaraka ili kujilipa deni ambalo inadaiwa aliikopesha Simba USD 300,000.
2. Nyaraka za uongo
Walitumia nyaraka za uongo ili kulipa deni kutoka benki ya CRDB.
3. Kutakatisha fedha 
Tarehe tofauti Aveva na Kaburu walikula njama za kutakatisha fedha UDS 300000.
4. Kutakatisha fedha
Aveva alijipatia fedha kutoka Barclays bank tawi la Mikocheni.
5. Kutakatisha fedha Kaburu
Kaburu alimsaidia Aveva kupata pesa USD 300,000 kutoka Barclays Bank tawi la Mikocheni

USIKOSE HABARI HII BAADA YA KUMPA MKATABA MPYA NGOMA SASA YANGA WAMALIZANA NA MTAALAM WA KUPASIA NYAVU BONYEZA HAPA KWA FULL STORI YANGA HAWATAKI UTANI WAMPA MKATABA WA MIAKA 2 MTAALAMU WA KUZIFUMANIA NYAVU

No comments:
Write comments