Sunday, 11 June 2017

KITUO CHA RUNINGA NCHINI URENO CHA FICHUA SIRI NZITO KUMHUSU RONALDO


Staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo imeelezwa amejaaliwa watoto wawili mapacha.

Taarifa zinaeleza pamoja na hivyo, Ronaldo ameendelea kufanya jambo hilo siri kama ilivyo kwa mtoto wake wa kwanza, Ronaldo Jr.

Runinga ya Ureno kupitia channel yake ya SIC, imesema watoto hao wawili, mmoja wa kiume na mwingine wa kike wamepewa majina ya Eva na Mateo.

Lakini mambo yameendelea kuwa siri na Ronaldo hajasema lolote.


Ronaldo hajawahi kumtaja mama wa mtoto wake wa kiume na sasa taarifa zinaendelea kusambaa naye akiendelea kuwa kimya.

Kwa sasa yuko na mpenzi wake ni mrembo wa Kihispania aitwaye Georgina Rodriguez ambaye hivi karibuni ilielezwa kuwa ni mjamzito.

Lakini runinga hiyo ya kwao Ureno, imeibua mambo mampya kabisa ambayo hayakuwa yamewahi kusikika

No comments:
Write comments