Saturday, 10 June 2017

KUNANI PALEE YANGA,AZAM WAWAPIGA TENA BAO KWA USAJILI HUU


http://i2.wp.com/soka360.co.tz/wp-content/uploads/IMG_3121.jpgKlabu ya Azan FC imeendelea kufanya yake baada ya kumsajili kiungo kutoka Mbao FC.

Salmini Hoza ndiye alikuwa akifanya kazi ya ukabaji na kupanga mashambulizi ya Mbao FC na alikuwa akiwaniwa na Yanga lakini tayari amesaini mkataba wa miaka miwili na Azam FC.


Hoza anakuwa mchezaji wa tatu aliyekuwa akitakiwa na Yanga lakini ametua Azam FC.

Awali, Waziri Junior wa Toto African alifika hadi makao makuu ya Yanga na kupiga picha na kombe la ubingwa,

Pili ni Mbaraka Yusuf wa Kagera Sugar ambaye ilibaki kidogo atue Yanga, naye kasajili Azam FC.

No comments:
Write comments