Mwanafunzi
wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 13 anayesoma Shule ya Msingi
Kipanga wilayani Tanganyika mkoa wa Katavi, amebakwa hadi kufa na watu
wasiojulikana, ambao waliutupa mwili wake korongoni.
Kaimu
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Benedict Mapujila alisema kitendo
hicho cha kikatili ni cha juzi ya saa 11:30 kijijini humo . Alisema siku
ya tukio hilo, mwanafunzi huyo wa kike aliondoka nyumbani kwao kama
kawaida yake kwenda shule.
Hata
hivyo, hakurudi tena kwao na kusababisha wasiwasi mkubwa kwa wazazi
wake, kwa kuwa hakuwa na tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani.
Wazazi
wake walikuwa na wasiwasi mkubwa kwa binti yao kuchelewa kurudi
nyumbani, hivyo waliamua kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji chao.
Viongozi hao wa kijiji na wananchi, walianza kumsaka binti huyo kwenye maeneo mbalimbali bila kukata tamaa.
“Ilipofika
saa kumi na moja na nusu ya jioni waliukuta mwili wa mwanafunzi huyo
ukiwa umetupwa korongoni na kubaini kuwa alikuwa amebakwa huku sehemu
zake za siri zikiwa zimeharibika vibaya,“ alisisitiza .
Alisema
chanzo cha kifo cha mwanafunzi huyo wa kike, kilisababishwa na kuvuja
kwa damu nyingi baada ya kufanyiwa ukatili huo na watu ambao
hawajafahamika.
Kamanda huyo alisema hakuna aliyekamatwa kuhusu tukio hilo na jeshi la polisi linaendelea kusaka wahalifu hao.
No comments:
Write comments