Jana katika kanisa la Ufufuo na Uzima Yule askofu machachari Askofu Gwajima
amejibu mashambulizi ya hotuba ya RC wa Dar Es Salaam yaliyofanyika
television ya Star TV majuma kadhaa yaliyopita. Amechambua hotuba yote
aliyofanya RC pale Star TV, ameeleza elimu ya Nape Nnauye, amechambua
tukio la uvamizi pale Clouds FM na akaeleze uhalali wa jina la Bashite
Kwa RC. Askofu Gwajima ameshusha nondo zake za kutosha kudhihirisha kuwa
muhusika wa hotuba jina lake halali ni Bashite. Ameenda mbali na kudai
kuwa hata namba za simu za baba yake kwenye miamala ya fedha
zimesajiliwa kwa jina la Bashite. Na akaitaja namba husika. Anasema
kabla sakata halijapamba moto bila wao kushtukia aliruka had mwanza na
ana picha alizopiga kwenye rejesta za shule ya msingi na sekondari na
majina ya muhusika yalikuwa ni Bashite. Pia askofu Gwajima anasema wiki
iliyopita aliwasiliana na Anthony Diallo kumuuliza kwa nin aliruhusu
kipindi cha kumdhalilisha. Askofu anasema Mh Diallo alimjibu kuwa
aliweza kumruhusu kumpa kipindi kwa kuwa Bashite alimuambia kuwa nataka
kuonyesha vyeti kwa watanzania na hivyo Diallo akaona ni jambo jema.
Askofu anasema hata baada ya kipindi Mh Diallo alishangaa kwa sababu
Bashite hakufanya kama alivyoomba. Askofu akaonyesha ujumbe mfupi wa
simu uliotoka kwa Diallo.
No comments:
Write comments