Kipa
Aishi Manula amethibitisha kwa mdomo wake kuwa anaondoka Azam FC na
kutua Simba huku akitaja sababu tatu za kuchukua uamuzi huo.
Kipa
huyo amesema hatasaini mkataba mpya na timu hiyo baada ya huu wa sasa
unaoisha Julai 31, mwaka huu kumalizika, na chaguo lake la kwanza ni
kutua Simba ambayo imeshamuandalia mkataba wa miaka miwili.
Manula
amesema anaondoka Azam kutokana na mabosi wa timu hiyo kutothamini kile
anachokifanya, pia dau dogo la usajili pamoja na timu hiyo kutokuwa na
nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.
“Sitasaini
mkataba mpya na Azam baada ya huu wa sasa kufikia tamati Julai 31,
mwaka huu, naamua kuondoka kwa sababu viongozi hawathamini uwezo wangu,
kwa sababu licha ya kujitoa kwa uwezo mkubwa lakini eti wananiwekea dau
la usajili chini ya milioni 20, hiyo inadhihirisha wazi kwamba hawajali
ninachokifanya.
“Niwe
muwazi kwamba mimi nilikuwa nacheza Azam kwa mapenzi yangu yote bila ya
kuangalia juu ya kile ninachokipata lakini kwa hili ambalo
wamenifanyia, naona kabisa siwezi kuendelea kucheza hapa, kwa sababu
thamani yangu wameishusha sana tofauti na ambavyo nilikuwa nafikiria.
“Lakini
pia naondoka Azam kwa sababu timu haishiriki michuano ya kimataifa kwa
msimu ujao, kwa hapa nilipofikia siwezi kucheza timu ambayo haishiriki
michuano ya kimataifa, ukiangalia mimi ni kipa wa timu ya taifa, hivyo
ni lazima nionekane na sehemu kubwa ya Afrika.
“Najua
kuna timu zinanifuatilia na baadhi yao tayari nimeanza kuzungumza nazo.
Lakini kipengele cha kwanza ambacho nimekiweka ni lazima nihakikishiwe
nafasi ya kuanza ndani ya kikosi cha kwanza halafu ndiyo mambo mengine
yafuate,” alisema Manula.
Tayari Manula amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili na ameondoka rasmi Azam FC ambayo alianza kujulikana akiwa nayo
No comments:
Write comments