Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza operesheni
maalumu ijulikanayo kama Ondoa Msaliti Buguruni (OMB) kwa lengo la
kutatua mgogoro unaokikabili Chama cha Wananchi (CUF).
Operesheni hiyo ya kidemokrasia imeanza rasmi jana Julai 10, ambapo vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimelenga kumuunga
mkono Katibu wa CUF, Maalim Seif.
Akizungumza leo wakati wa kutangaza operesheni hiyo, Makamu Mwenyekiti
wa Chadema kanda ya Pwani, Saed Kubenea amesema kuwa mgogoro huo una
athari kubwa kwa vyama vya upinzani hivyo wameamua kuungana pamoja ili
kuimarisha vyama vya upinzani chini ya mwavuli wa Ukawa.
Kubenea ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, ameeleza kuwa baada ya kukaa na
viongozi wa CUF ili kujua kiini cha mgogoro huo wamebaini kuwa siyo
mgogoro ndani ya chama, bali unachochewa na CCM wanaomtumia Profesa
Lipumba ambaye wamemuita kama ni msaliti.
"Sisi kama Chadema tumeamua kuwasaidia viongozi na wanachama wa CUF
kumuondoa msaliti Lipumba Buguruni na kutupa nguo zake na viongozi
halali wa CUF watarudi Buguruni, "amesema Kubenea.
Kadhalika amesema pamoja na mambo mengine, chama kimeazimia kuwa mameya
wa Manispaa zote za Jiji la Dar es Salaam wasitoe ushirikiano kwa
viongozi wenye ushirikiano na Profesa Lipumba.
KAMA ULIPITWA NA TUKIO LA HALIMA MDEE KUACHIWA KWA DHAMANA HAPO JANA BONYEZA HAPA CHINI UJIONEE MWENYEWE ALICHOKIONGEA MBOWE BAADA YA HALIMA MDEE KUACHIWA NA MAHAKAMA KWA DHAMANA:-
VIDEO:ALICHOKISEMA MBOWE BAADA YA HALIMA MDEE KUACHIWA KWA DHAMANA
Monday, 10 July 2017
CHADEMA WATANGAZA OPERESHENI MAALUMU IJULIKANAYO KAMA ONDOA MSALITI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments