Klabu ya Simba imepanga kuwaacha nyota wake watatu wa kimataifa kwa utovu wa nidhamu na kushuka kwa viwango vyao.
Nyota hao ni Jamvier Bokungu raia wa DR Congo na Fredrick Blagnon,
mshambuliaji raia wa Ivory Coast wanaodaiwa kushuka viwango. Beki
Mganda, Juuko Murshid yeye anatemwa kutokana na kudaiwa kukosa nidhamu
licha ya uwezo wake uwanjani kuwa mkubwa zaidi.
Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Usajili Simba alisema wanaandalia
wachezaji hao barua za kuwataarifu waanze kusaka timu za kujiunga nazo
kabla msimu wa usajili haujapita.
“Kamati yetu imepanga kuachana na wachezaji hao kutokana na usajili
tulioufanya. Mfano wa beki wa kulia tumemsajili Shomari Kapombe na Ally
Shomari, Hapo Bokungu hana nafasi.
Pia kuna mshambuliaji tutamtangaza hivi karibuni kumrithi Blagnon na
beki wa kati,” alisema. Alisema mbali na nyota hao wa kigeni, pia kuna
baadhi ya wachezaji wazawa watawaacha baada ya mchango wao kuwa mdogo
klabuni.
Wachezaji hao ni beki wa kulia, Juma Hamad,Pastory Athanas, Jamali
Mnyate na Novaty Lufunga walioruhusiwa kutafuta timu msimu ujao na
wengine wamemaliza mikataba yao. Simba iko katika mikakati ya
kumwongezea mkataba kiungo wake mkabaji raia wa Ghana, James Kotei
ambaye sasa ni mchezaji huru
SOMA NA HABARI HII KUTOKA UKAWA-:CHADEMA WATANGAZA OPERESHENI MAALUMU IJULIKANAYO KAMA ONDOA MSALITI
Monday, 10 July 2017
SIMBA WATAJA SABABU ZA KUWAACHA NYOTA WAO.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments