Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi tayari ameanza mazoezi na wenzake na ameonekana si mgeni katika kikosi hicho.
Simba
imeweka kambi jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini, kujiandaa na
msimu mpya wa 2017-18 na kikosi chake kitaanza kuonekana hadharani kwa
mara ya kwanza wakivaa Rayon ya Rwanda kwenye Uwanja wa Taifa siku ya
tamasha la Simba Day.
Jambo
la pili ambalo ameonyesha Okwi baada ya kuanza mazoezi, anaonekana ni
mtu aliyekuwa akijifua au alifanya mazoezi kutokana na kuwa katika
kikosi cha timu ya taifa.
Kwani anaonekana kuwa fiti na mwepesi licha ya kwamba mazoezi waliyofanya ni yale ya kupasha misuli.
“Okwi anaonekana yuko vizuri tu na ameonekana ni mwenye furaha baada ya kuungana nasi,” alisema mmoja wa wachezaji wa Simba.
Kitu
kingine kizuri ni Okwi kupokelewa na wachezaji wa Simba wa zamani
wakiwemo wale wapya ambao pia anawajua kwa kuwa aliwahi kukutana nao
akiwa Simba na wao wakiwa na timu zao kam Azam FC, Mtibwa Sugar na
kadhalika.
No comments:
Write comments