Mshambuliaji Donald Ngoma anaweza kuanza mazoezi na kikosi cha Yanga.
Ngona anaweza kuanza mazoezi baada ya madaktari waliokuwa wakimtibu goti nchini Afrika Kusini, kumruhusu kuanza mazoezi.
Mzimbabwe
huyo, alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na majeraha hayo
yaliyosababisha azikose mechi za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara na
zile za kimataifa.
Kurejea kwa Ngoma kutaiimarisha safu ya ushambuliaji ya Yanga inayoundwa na Obrey Chirwa, Simon Msuva na Amissi Tambwe.
Katibu
Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amesema mshambuliaji huyo anatarajiwa
kuanza mazoezi wiki hii baada ya kurejea nchini akitokea Afrika Kusini
alipokwenda kufanyiwa vipimo vya mwisho kabla ya kuruhusiwa.
Mkwasa
alisema mshambuliaji huyo alipumzishwa na madaktari hao kwa muda wa
miezi minne ambayo tayari imemalizika, hivyo yupo fiti hivi sasa kwa
ajili ya mapambano.
Aliongeza
kuwa, timu yao inaendelea na mazoezi ya gym na mazoezi ya uwanjani kila
siku asubuhi na jioni kwa muda wa wiki mbili kabla ya kucheza mechi za
kirafiki.
"Ni
habari njema kwa mashabiki wa Yanga kuwa mshambuliaji wao Ngoma yupo
fiti baada ya kupona goti lake. Madaktari wa Afrika Kusini wamemruhusu
kuanza mazoezi.
"Anatarajiwa
kuanza mazoezi mapema wiki hii mara baada ya kurejea kutoka Afrika
Kusini alipokwenda kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya mwisho.
"Kurejea
kwa mshambuliaji huyo kutaimarisha kikosi chetu kwa ajili ya mechi ya
Ngao ya Jamii, ligi kuu na michuano ya kimataifa Afrika tutakayoshiriki
mwakani," alisema Mkwasa.
USIPITWE NA HABARI HII YA MUUGUZI ALIYEMCHOMA MGONJWA SINDANO YA USINGIZI NA KUMTENDEA KITENDO CHA KINYAMA BONYEZA HAPA CHINI KUJIONEA MWENYEWE
MUUGUZI AMFANYIA MGONJWA KITENDO CHA KINYAMA BAADA YA KUMCHOMA SINDANO...............JIONEE MWENYEWE KITENDO ALICHOKIFANYA
USIPITWE NA HABARI HII YA MUUGUZI ALIYEMCHOMA MGONJWA SINDANO YA USINGIZI NA KUMTENDEA KITENDO CHA KINYAMA BONYEZA HAPA CHINI KUJIONEA MWENYEWE
MUUGUZI AMFANYIA MGONJWA KITENDO CHA KINYAMA BAADA YA KUMCHOMA SINDANO...............JIONEE MWENYEWE KITENDO ALICHOKIFANYA
No comments:
Write comments