Muuguzi
anayefanya kazi Kituo cha Afya Kata ya Igurubi Wilaya ya Igunga mkoani
Tabora, Damian Mgaya (26) anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma ya kumbaka
binti wa miaka 18 mkazi wa kitongoji cha Mwagala B, Kijiji cha Mwagala.
Mtendaji
wa Kata ya Igurubi, Ntemi James alisema uhalifu huo umefanyika Julai
14, mwaka huu saa 8 hadi alfajiri wakati binti huyo akimuuguza mama
yake, Tatu Simbi ambaye amelazwa katika kituo hicho cha afya baada ya
kushambuliwa kwa kipigo na mume wake.
James
alidai mtuhumiwa alimpokea mama wa binti huyo akiwa hoi na ndipo
alimpatia matibabu kisha kumlaza katika kituo hicho cha afya huku
akimchoma sindano ya usingizi ambayo ilisababisha mama huyo kupitiwa na
usingizi.
Mtendaji
huyo alidai kuwa muuguzi Damian alipoona mama wa binti huyo amelala,
alimwambia waende wote chumba kingine ili akachukue dawa ya mama yake;
lakini hata hivyo hakumpa dawa na badala yake alimwambia amchome sindano
ili asipate maradhi kwa kuwa mazingira ya hospitali sio mazuri.
Baada
ya kuambiwa hivyo, binti huyo alikubali kuchomwa sindano mbili na
alipochomwa sindano ya kwanza aliishiwa nguvu na alipochomwa sindano ya
pili alianguka na kupitiwa na usingizi hadi asubuhi.
Alisema
baada ya kuona amelala pasipokuwa na fahamu, muuguzi huyo alianza
kumbaka hadi alfajiri alipoamshwa na mama yake huku yeye akiwa
hajitambui kutokana na maumivu aliyokuwa akiyasikia sehemu zake za siri
na mwili wote.
Kaimu
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bonaventura Kalumbete alithibitisha
kubakwa kwa binti huyo na muuguzi huyo na kueleza kuwa baada ya kupata
taarifa hiyo, alituma timu ya wataalamu ambayo ilibaini binti huyo
kubakwa na amelazwa kwenye kituo hicho na hali yake ni mbaya kwani
hawezi kutembea.
Aidha,
Dk Kalumbete alisema uchunguzi wa awali unaonesha binti huyo alichomwa
sindano wakati alikuwa hata haumwi na hizo dawa nazo zimechangia
kumsababishia kushindwa kutembea huku akiahidi kuwa baada ya uchunguzi,
muuguzi huyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
USIKOSE KUISOMA HABARI YA MSHAMBULIAJI WA YANGA ALIYEUMBULIWA NA MADAKTARI KWA KUBONYEZA HAPA CHINI
DONALD NGOMA ALIAMSHA DUDE JANGWANI
No comments:
Write comments