Sunday, 16 July 2017

SIMBA SPORT CLUB WAANZA MAANDALIZI YA MSIMU UJAO

Image result for SIMBA SC
KLABU ya Simba ya jijini Dar es Salaam, itaondoka Jumanne ya Julai 18, mwaka huu kwenda Afrika Kusini kuweka kambi ya wiki tatu kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.
Simba ambayo imefanya usajili wa wachezaji tisa mpaka sasa, imebakiza usajili wa wachezaji wawili tu ili hesabu ya usajili ifungwe.
Habari kutoka Simba zinasema kuwa, Jumanne  itaondoka na wachezaji wake wote ambao hawapo kwenye majukumu ya timu ya taifa ambapo mjumbe mmoja wa kamati ya utendaji klabuni hapo alisema kambi hiyo imefadhiliwa na mwanachama wa klabu hiyo na mfadhili, Mohamed Dewji ‘Mo’.
Ikiwa Afrika Kusini, Simba itacheza mechi tatu za kirafiki na timu za huko na itarejea nchini Agosti 5 kwa Ajili ya maandalizi ya mwisho ya Simba Day itakayofanyika Agosti 8.
Wachezaji ambao mpaka sasa Simba imewasajili ni magolikipa wawili Aishi Manula na Emmanuel Mseja,  mabeki Shomary Kapombe,  Ally Shomary,  Jamali Mwambeleko,  Salim Mbonde na Yusuph Mlipili, huku washambuliaji wakiwa ni John Bocco na Emmanuel Okwi.
Wachezaji wa Simba ambao wapo kwenye majukumu ya timu ya taifa ni Aishi Manula, Shomary Kapombe, Salim Mbonde, Mzamiru Yassin, Said Ndemla, Shiza Kichuya na John Bocco ambao wataungana na wenzao kwenye kambi Julai 24 baada ya mechi dhidi ya Rwanda wikiendi ijayo.

No comments:
Write comments