TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
______________
Benchi la ufundi la klabu ya Simba,chini ya kocha wake mkuu Joseph Omog limefanya marekebisho kwenye eneo la unahodha wa timu.
Katika
marekebisho hayo yaliyoridhiwa na uongozi wa klabu,beki wa kimataifa
Mzimbabwe Method Mwanjale ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa timu ya
Simba,akichukua nafasi ya Jonas Mkude atakaendelea kuwa mchezaji
mwandamizi kwenye kikosi hicho,ambacho kwa sasa kipo nchini Afrika
kusini kujiandaa na msimu mpya unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.
Kwenye
mabadiliko hayo ya kawaida, benchi la ufundi pia limewateua Mchezaji
bora wa ligi kuu ya Tanzania na klabu ya Simba kwa msimu huu,Mohammed
Hussein(Tshabalala)na John Raphael Boko kuwa manahodha wasaidizi wa timu
hiyo.
Klabu
inamshukuru sana Nahodha wake kwenye msimu uliopita na mchezaji wake
mwandamizi,Jonas Mkude kwa kazi nzuri alioifanya muda wote alipokuwa
Nahodha wa Timu.
Kwa
sasa kikosi chetu kinaendelea na mazoezi na kila kitu kinakwenda vema
huko kambini Eden Vale Johannesburg nchini Afrika kusini.
IMETOLEWA NA..
HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI WA SIMBA SC
SIMBA NGUVU MOJA
No comments:
Write comments