Watafiti kutoka nchini Marekani wamesema kuwa wamekamilisha
majaribio yaliyofanikiwa kwa wasichana nchini humo ya pete inayowekwa
sehemu za siri za mwanamke kwa lengo la kuzuia maambukizi ya Virusi Vya
Ukimwi (VVU).
Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, watafiti hao ambao ni jopo la
wataalam wa masuala ya afya wamesema kuwa zoezi hilo linahamia kwa
mabinti barani Afrika.
Zoezi hilo hufanywa kwa kuweka pete ya plastiki ukeni, pete ambayo
huwekewa dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi, kwa lugha ya
kiingereza Anti-Retroviral (ARV) na hubadilishwa mara moja kwa mwezi.
Wataalam hao wanadai kuwa utafiti uliofanywa kwa mabinti wa Marekani kwa muda wa miezi sita ulionesha mafanikio makubwa.
Utafiti huo unatokana na utafutaji wa njia ya wanawake kuweza kujilinda dhidi ya virusi vya ukimwi wakati wa kujamiiana bila kutegemea wanaume kuvaa mipira (condoms).
Ripoti inaonesha kuwa asilimia hamsini ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi yako kwa wasichana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 na kwamba takribani jumla ya vijana na mabinti 1,000 huambukizwa virusi vya ukimwi katika ukanda wa Jangwa la Sahara
No comments:
Write comments