Kwa kuwa kiungo Haruna Niyonzima, rasmi amemaliza mkataba wake na Yanga, Simba iko huru kumtambulisha wakati wowote ule.
Simba
imemsajili Niyonzima raia wa Rwanda lakini imekuwa ikificha mambo kwa
hofu ya kuonekana imemsajili mchezaji huyo kabla mkataba kwisha.
Baada
ya mkataba wake kwisha maana yake, Simba inaweza kumtangaza Niyonzima
kuanzia leo, kesho au keshokutwa na baada ya hapo itakuwa huru kuendelea
na shughuli zake.
Simba ilimsajili Niyonzima baada ya Yanga kushindwa kumalizana naye na kumpa ruhusa kuendelea na kusaka timu kokote anakotaka.
Mnyarwanda huyo ameichezea Yanga kwa mafanikio makubwa huku akiwa ni injini ya uchezeshaji.
No comments:
Write comments