Sahau
kuhusiana na Kipa Ally Mustapha ‘Barthez’ aliyesajiliwa na Singida
United, timu hiyo imemweka mkononi kiungo mshambuliaji Deus Kaseke
aliyemaliza mkataba na Yanga.
Kocha
wa Singida United, Hans van Der Pluijm raia wa Uholanzi, ameweka wazi
kuwa ana furaha kubwa msimu ujao kufanya kazi na Kaseke aliyewahi
kufanya kazi wakiwa Yanga msimu uliopita.
Jana
Ijumaa Kaseke aliliambia Championi Jumamosi kuwa; “Muda wowote nasaini
Singida United, halafu kesho (leo) naenda Mwanza kambini kuungana na
wenzangu, hii imekuja baada ya kushindwana na Yanga katika kuongeza
mkataba.”
Kaseke
anasaini miaka miwili kucheza Singida United ambako ataungana na
Barthez, ambaye walicheza wote msimu ulioita Yanga na kutwaa ubingwa wa
Ligi Kuu Bara.
Pluijm ameliambia gazeti hili kwamba: "Kaseke yupo njiani anakuja Singida United, naweza kusema huyu ni kati ya vijana ambao wanajielewa na wanajua majukumu yao wawapo uwanjani, nafurahi kufanya naye kazi tangu nikiwa Yanga na sasa anakuja huku
No comments:
Write comments