Siku
chache baada ya kiungo wa Simba, Said Ndemla kwenda Sweden kufanya
majaribio katika Klabu ya AFC, mshambuliaji wa timu hiyo, Shiza Kichuya
anaweza akapata shavu la kucheza soka nchini Misri.
Taarifa
kutoka ndani ya Simba zinasema klabu moja ya Misri inamtaka Kichuya ili
imsajili kwa ajili ya kuichezea timu yao na sasa wapo katika
mazungumzo.
Bado mazungumzo ya Simba na klabu hiyo yanaendelea na wakifikia muafaka muda wowote Kichuya ataondoka kwenda nchini humo.
“Kuna
timu ya Misri kupitia wakala aliyemuona Kichuya kwenye ligi na kufanya
mawasiliano na sisi na tayari kuna barua wameleta wakimtaka Kichuya.
“Kuna
dau ambalo wamelipendekeza ili waweze kumsajili Kichuya lakini sisi
hatujakubaliana nalo, hivyo tupo katika mazungumzo ya kuweza kufikia
makubaliano lakini tunataka waongeze dau.
“Hata
hivyo, itabidi tumuachie Kichuya akacheze soka la kulipwa kwani kumzuia
mchezaji kwa sasa ni sawa na bure, kwani amebakiza mwaka mmoja katika
mkataba wake na hatutaki baadaye aende bure.
“Maongezi
yanaonekana kuendelea vizuri na wakati wowote mambo yatakaa sawa kwani
klabu yenyewe haimuhitaji mchezaji kwa ajili ya majaribio na badala yake
kwenda kucheza moja kwa moja,” alisema bosi huyo.
No comments:
Write comments