Kiungo
mkabaji wa Mbabane Swallows ya Swaziland, Papy Kabamba Tshishimbi, jana
asubuhi aliondoka nchini kurudi kwao DR Congo, lakini ameiachia mzigo
mzito Yanga iliyofikia makubaliano naye ya kumsajili.
Hali
hiyo, imekuja ikiwa ni siku chache tangu kiungo huyo atue nchini na
kufanya mazungumzo na Yanga kwa ajili ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja
waliokubaliana naye.
Tshishimbi
raia wa DR Congo, tayari amefanyiwa vipimo vya afya na Yanga ambavyo
vimeonyesha amefuzu, hivyo yupo kamili kwa ajili ya kuichezea timu hiyo
bingwa wa Ligi Kuu Bara.
Taarifa
za kuaminika kutoka Yanga zinaeleza, kiungo huyo amemalizana kila kitu
na klabu hiyo lakini kilichobaki ni Yanga kumalizana na Mbabane kwani
Tshishimbi bado ana mkataba nao wa miezi minne.
Imeelezwa
kuwa, kiungo atarejea nchini kujiunga na Yanga mara baada ya pande hizo
mbili kumalizana katika mkataba wake wa miezi minne aliyoibakisha
Mbabane.
Yanga
imedai makubaliano na Mbabane yatafikiwa muafaka hivi karibuni kutokana
na klabu hiyo ya Swaziland kuonyesha nia ya kumuachia Tshishimbi baada
ya kumruhusu aje nchini kufanya mazungumzo na Wanajangwani.
“Kila
kitu kimekamilika kwa Tshishimbi kwa maana ya dau la usajili, mshahara
na mahitaji mengine anayoyataka tumekubaliana naye, alikuja kwa ajili ya
kazi hiyo pekee ambayo tayari tumekamilisha.
“Alikuja
kwa ruhusa ya viongozi wake na sisi baada ya mazungumzo akaondoka
kwenda kwao, kazi iliyobaki ni sisi kuzungumza na Mbabane ili tumalizane
nao.
No comments:
Write comments