Tetesi na mabishano yamezidi kuchukua nafasi kubwa kwenye
vijiwe mbalimbali na sehemu nyingine nyingi mitaani watu wakibishana
kuhusu beki wa kushoto wa Azam na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa
Stars’ Gadiel Michael wengine wakidai kwamba anaihama klabu yake ya Azam
na kujkiunga na mabingwa wa VPL Yanga wakati wapo wanaobisha.
Shaffihdauda.co.tz ikaona ni vyema
kumtafuta mwenyewe Gadiel ili azungumzie ukweli kuhusu suala hili na
kumaliza utata uliopo, timu ya shaffihdauda.co.tz ikafanikiwa kufanya
mahojiano maalum na Gadiel jijini Mwanza ambako alikuwa kambini na timu
ya taifa kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano utakaochezwa leo
Juali 22, 2017 dhidi ya Rwanda kuwania kufuzu fainali za CHAN 2018.
“Hizo taarifa zipo, watu wengi wanasema hivi na vile mara mimi
nakwenda Yanga, lakini kwangu mimi siwezi kuliweka wazi hilo kwa sababu
bado nina mkataba na Azam, mkataba wangu na Azam utakapomalizika ndio
tutajua nabaki Azam au naenda Yanga lakini kwa sasa hivi siwezi kusema
chochote kwa sababu bado nina mkataba na Azam na bado nipo Azam,” Gadiel
Michael.
“Mkabata wangu na Azam umebakiza miezi miezi mitano (5) (hadi mwezi
Disemba) chochote kinaweza kutokea kuanzia hapo lakini kwa sasa siwezi
kusema lolote kwa sababu nipo ndani ya mkataba na Azam.”
Kwa sasa Gadiel yupo kwenye kiwango cha juu na amefanikiwa kucheza
mechi zote za Stars ambazo Mohamed Hussein hajacheza tangu alivyopata
majeraha kwenye fainali ya kombe la Azam Sports Federation Mei 27, 2017
dhidi ya Mbao FC.
Gadiel alifanya vizuri kuanzia mechi ya Stars dhidi ya Lethoto
iliyochezwa uwanja wa Azam Complex kabla ya michuano ya COSAFA 2017
nchini Afrika Kusini ambapo alicheza mechi zote na kufanya vyema.
Alikuwepo pia kwenye kikosi kilichocheza dhidi ya Rwanda kwenye mechi ya
kwanza kuwania kufuzu michuano ya CHAN 2018 wakati Stars ilipotoka sare
ya goli 1-1 kwenye uwanja CCM Kirumba, Mwanza.
Inaelezwa kwamba, tayari Yanga imeshamalizana na Gadiel huku nyota
huyo akisubiri kumaliza mkataba wake na Azam na huenda akajiunga na
mabingwa hao wa VPL katika dirisha dogo la usajili. Yanga wanataka
Gadiel akasaidiane na Haji Mwinyi katika nafasi ya ulinzi wa kushoto
kutokana na klabu hiyo kuachana na Oscar Joshua ambaye mkataba wake
umemalizika.
HAJI MANARA ACHOKI ATUMA DONGO ZIPO KWA YANGA JIONE MWENYEWE KWA KUBONYEZA HAPO CHINI
HAJI MANARA ASHINDWA KUVUMILIA ATOA YA MOYONI ATUMA KOMBORA LINGINE KWA WATANI WAO WA JADI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments