Samatta amethibitisha hilo leo japo amekataa kutaja ni klabu gani hasa ambayo inahitaji huduma yake lakini amesisitiza kuwa inaweza kuwa ni dirisha dogo la usajili la mwezi Januari au lile dirisha kubwa la kiangazi mwezi wa sita.
“Nataka kuondoka Genk nahisi ni muda sahihi wa kucheza ligi nyingine kubwa hususani ligi ya England na wakala wangu analifanyia kazi hilo. Inaweza ikawa Januari ama mwezi wa sita lakini lazima niondoke kama sio EPL basi hata Serie A”, amesema Samatta.
Samatta amekuwa kwenye kiwango kizuri tangu ajiunge na KRC Genk ambapo amefanikiwa kufunga mabao 22 hadi sasa. Nahodha huyo wa Stars yupo nchini na aliingoza Stars kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi siku ya Jumamosi na timu hizo zilifungana bao 1-1.
Katika mchezo huo Samatta aliumia kipindi cha pili akalazimika kutolewa lakini amesema anaendelea vizuri.
No comments:
Write comments