Thursday, 5 October 2017

VINARA WA LIGI KUU TANZANIA BARA WEKUNDU WA MSIMBAZI SIMBA WAPELEEKA KILIO CHAO KWA CHAMA CAHA MAPINDUZI CCM

Related imageBaada ya Simba kushinda kwa bao 1-0 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Dodoma FC, klabu hiyo imekiomba chama tawala cha CCM kufanya ukarabati katika viwanja inavyovimiliki.

Simba ilishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Said Ndemla nje ya 18 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema mechi ilikuwa nzuri lakini uwanja ulikuwa tatizo kubwa.

“Mechi ilikuwa nzuri na timu yetu ilicheza vizuri, Dodoma FC pia walicheza vizuri.

“Lakini nikiombe Chama cha Mapinduzi kufanya ukarabati katika viwanja vyake ili kurahisisha uchezaji,” alisema.

Simba imecheza mfululizo katika viwanja vinne vyote vinavyomilikiwa na CCM na vitatu kati yake vilikuwa dhoofu el hali.

Mechi ya kwanza ilikuwa dhidi ya Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba ambao ulionekana ni wenye nafuu. Baada ya hapo ikasafiri hadi Tabora kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Milambo. Mechi ilichezwa kwenye Uwanja wa CCM na uwanja ulikuwa hoi.


Mechi ya tatu Simba walicheza na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United kwenye Uwanja wa CCM Kambarage ambao ulikuwa dhoofu kwelikweli na baada ya hapo walisafiri hadi Dodoma kucheza mechi hiyo ya kirafiki kwenye Uwanja wa Jamhuri.

No comments:
Write comments