Friday 8 September 2017

WANAFUNZI KATIKA CHUO CHA UANDUSHI NA UTANGAZAJI ARUSHA WALALAMIKIA HUDUMA YA KUSAJILI LAINI ZA WANACHUO

Wanafunzi   katika  chuo  cha uandishi wa habari na utangazaji  Arusha(A.J.T.C) wametoa malalamiko yao kwa kampuni  ya Vodacom mapema leo hii wakilalamikia huduma ya kusajili laini za chuo inayotolewa na mawakala wa kampuni hiyo.
Kelly Luna ni mmoja wa wanafunzi katika chuo hicho anayelalamikia huduma hizo akielekeza malalamiko yake kwa mawakala  wakampuni  hiyo kuwa hawajui kuelekeza wateja wao jinsi ya kujiunga na vifurushi hivyo vya wanachuo na pindi wanapowauliza menyu ya kujiunga na vifurishi vya wanachuo wanakosa majibu ya kuwapa na hivyo kuhisi wanaibiwa kwani watakua wanasajili laini za kawaida nasiyo za wanachuo.
Naye bi   Lilian Deidan ambaye ni miongoni mwa wanafunzi  wa chuo hicho  cha  uandishi  wa  habari  na utangazaji  Arusha  ambaye  amesajili laini hizo  za wanachuo amesema bado hajaona tofauti yoyote ya laini za voda  za  chuo na laini za kawaida kwani alivosajili aliambiwa angoje masaa 24 na atakua kaunganishwa na vifurushi vya chuo lakini muda huo umeshapita na  bado hajaunganishwa.
Kwaupande wake  Bw Rashidi  Salim ambaye ni mmoja wa mawakala wa kampuni hiyo anayesajili laini hizo amesema kuhusiana na swala la kusajili laini na kuchukua muda mrefu na kutokuunganishwa na vifurushi vya chuo,hiyo ni kwazile namba ambazo zinabadilishwa kutoka namba za kawaida kwenda za chuo kwani ni lazima makao makuu warudie kuhakiki.
Ameongeza kuwa kwa wale wanafunzi  wanaosajili laini  mpya hakuna  usumbufu  wowote unaojitokeza kwa sasa na swala la kusuasua kwa mtandao lilitokea siku ya kwanza ya usajili ila kwa sasa mambo yako shwari kwani  wameshafanya marekebisho kwenye mtandao.

Vodacom ni moja ya kampuni kubwa ulimwenguni  inayotoa huduma za simu ya mkonono na imekuja na vifurushi vipya kwaajili ya wanachuo vinavyoanzia Tsh 500/= hadi 2000/= ambavyo ni vya siku hadi wiki na lengo la vifurushi hivi ni kuwapunguzia gharama wanavyuo na kuwapa ongezeko la vifurushi.

No comments:
Write comments