Wednesday, 15 November 2017

JANGWANI MAMBO SAFI KUPITA NA INJINI YA MTIBWA




Kiungo mwenye kiwango cha kuvutia Mtibwa Sugar, Mohamed Issa ‘Banka’ ambaye anawindwa na Yanga amesema kuwa yupo mbioni kumaliza mkataba wake.

Kiungo huyo amesema kuwa baada ya mkataba huo yupo tayari kwa sasa kutua kwenye klabu yoyote itakayomhitaji.

Banka ambaye alitua Mtibwa Sugar mwaka jana anaweza kuchezea nafasi tano uwanjani ambazo ni sita, saba, nane, kumi na kumi na moja ambazo zote anazimudu vyema.

Kiungo huyo amekuwa akizitoa udenda timu kubwa za Simba na Yanga kutokana na umahiri wake wa kulisakata kabumbu, hivyo lolote linaweza kutokea usajili wa dirisha dogo.

Banka alisema kuwa, anatarajia kumaliza mkataba wake na klabu yake hiyo ya sasa licha ya kutotaka kuweka wazi anamaliza lini lakini amesema anaweza kutua kokote.

“Nakaribia kumaliza mkataba wangu na Mtibwa hivi karibuni ila siwezi kusema ni lini na sijajua kama nitaongeza ama nitabaki.


“Mimi ni mchezaji nipo tayari kwenda timu yeyote inayonihitaji ijapokuwa siwezi sema ni timu gani zimenifuata hadi sasa kwa kuwa sihitaji kuweka wazi kila kitu hadi kikamilike lakini ieleweke kuwa kuna timu zinanitaka na siyo moja,” alisema Banka.

SOURCE: CHAMPIONI

No comments:
Write comments