Sunday, 25 March 2018

POGBA,SHAW WAMUWEKA MOURINHO KUTI KAVU


Image result for mourinhoHali imeanza kuwa si shwari ndani ya kikosi cha Manchester United kutokana na Kocha Jose Mourinho kutokuwa na mwenendo mzuri na baadhi ya wachezaji.

Mourinho ameripotiwa mara nyingi kutokuwa na maelewano na kiungo Mfaransa, Paul Pogba na hii imetokana na kutomtumia mchezaji huyo kwenye mechi kama siku za mwanzo.

Mbali na Pogba, Luke Shaw, naye ameunga orodha hiyo baada ya kuonekana kutoelewana pia na Mourinho. Shaw alitupiwa lawama na Mourinho baada ya mchezo dhidi ya Brighton FC walioshinda kwa mabao 2-0 kwenye Kombe la FA akilalamikia kuhusu kiwango chake.

Kitendo hicho kimelifanya benchi la ufundi la timu hiyo na baadhi ya wachezaji kuanza kuona taswira mbovu ya timu hiyo siku za usoni kutokana na Kocha huyo kuingia kwenye matatizo na wachezaji hao wa United.

Tetesi zinaeleza kuwa, baada ya Pogba kutaka kuondoka klabuni hapo, Shaw naye anaelezwa kuihama timu hiyo baada ya msimu huu kumalizika.

No comments:
Write comments