Monday 13 March 2017

Deni la umeme Z’bar, tume iundwe- Mbunge


Ushauri huo umetolewa na mbunge wa zamani wa Kikwajuni Parmukh Singh Hoogani, alipokuwa akizungumzia hatua ya Shirika la Umeme (Tanesco), kutoa siku 14 wadaiwa kulipa kabla ya kukata huduma wakiwamo Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO).
Alisema pamoja na ZECO kudaiwa na Tanesco kiasi cha Sh. bilioni 122 kama gharama za huduma ya umeme, lakini ZECO wanastahili kulipwa gharama za matumizi ya miundombinu ambayo imetumika kufikisha huduma hiyo.
Alisema deni la Tanesco la muda mrefu hatua ya kuunda tume itaweza kufahamu sababu ya ZECO kushindwa kulipa gharama za huduma ya umeme wakati wananchi wamekuwa wakilipia huduma hiyo.
“Wananchi Zanzibar tunapata huduma kwa kukopesha Shirika kwa sababu tunalipa kabla ya kutumia kupitia mita za TUKUZA haiwezekani shirika lishindwe kujiendesha kibiashara,” alisema Singh.
Alisema tume hiyo itaweza kuja na mapendekezo mwafaka ya kutafuta njia mbadala ya kumaliza deni la umeme na mpango kazi wa kulisaidia shirika kujiendesha kibiashara.
Alisema kabla ya Tanesco kukata huduma ya umeme Zanzibar, kunahitajika hekima na busara ili kulinda siasa za Muungano na maslahi ya Zanzibar na wananchi wake.
“Kama wananchi wa Zanzibar wanalipa huduma ya umeme tena kabla ya kutumia kuwanyima huduma kwa sababu ya deni la Tanesco na ZECO sio kuwatendea haki,”alisema Singh.
Alisema hivi karibuni ZECO wamefikia kufungiwa ofisi za makao makuu na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), kutokana na kudaiwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ambayo wamekuwa wakikusanya kama wakala wa serikali kupitia malipo ya umeme kutoka kwa wateja wake.
Aidha, alisema wakati umefika kwa Zanzibar kwenda kujifunza kwa nchi nyingine za visiwa zimeweza vipi kuwa na umeme wa uhakika wa kujitegemea badala ya kutegemea chanzo kimoja cha kuzalisha umeme

No comments:
Write comments