Mgombea Ugavana wa Jimbo la Kisumu amewaahidi wapiga kuwa kuwa ataweka
mazingira rafiki kwa wanaofanya biashara ya kuuza miili yao (makahaba)
na kuhakikisha wanapata faida endapo watamchagua katika uchaguzi mkuu
ujao.
Dkt. Hezron Mc’Obewa, ambaye anarusha karata yake ya ugavana katika
jimbo hilo kumng’oa kiongozi aliyepo sasa, Jack Ranguma aliyasema hayo
siku ya Jumanne alipokuatana na makahaba zaidi 300 katika Taasisi ya
Goan.
Dkt. Mc’Obewa alisema kuwa atashinikiza mikutano ya kimataifa iwe inafanyikia pia Kisumu ili makahaba hao waweze kupata soko.
“Watu hawa hulipa vizuri wanapokwenda nchi za ugenini, na
wafanyabiashara hao hupata hadi Ksh 200,000 kwa usiku mmoja” alisema
mgombea huyo. “Mikutano hii mikubwa ndiyo huleta wateja watakaowalipa
ninyi kwa viwango vywa kimataifa” aliongeza.
Mbali na ahadi hiyo iliyozua gumzo maeneo mengi, mgombea huyo amewaahidi
kuwa atahakikisha kunakuwapo ajira za kutosha ili watu wawe na fedha
kwenye mifuko yako.
“Biashara yenu ninyi itakuwa na faida kama wanaume watakuwa na fedha
mfukoni, na hii ndio sababu lazima tuhakikishe tunamaliza ukosefu wa
ajira” alisema Dkt. Mc’Obewa.
Mgombea huyo alisema kiongozi wa sasa wa jimbo hilo hawajali kabisa
makahaba hao ambao chini ya mwamvuli wa Kisumu Sex Workers Sacco. Hivyo
amewasihi kumchagua yeye ili waweze kufurahia biashara yao na
atahakikisha anaimarisha ulinzi dhidi yao.
“Wakati mwingine unapata mteja ambaye anakupakiza kwenye gari lake,
lakini usalama wako unakuwa ni mdogo, au unafayia kazi katika mazingira
machafu ambayo yanahatarisha afya yako. Haya yote ndiyo tunataka
yabadilike”, alisema.
Aidha, mgombea huyo aliwataka makahaba hao kujisajili katika Shirika la
Taifa la Bima ya Afya (NHIF) ili kuweza kupata huduma za kitabibu.
No comments:
Write comments