Kampuni ya Reli Tanzania imezindua rasmi huduma maalumu ya usafirishaji
wa shehena kwa njia ya reli kutoka dar es salaam kwenda Burundi kwa
kutumia train nzima(Block Train).
Akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza safari kwa treni hiyo , kaimu
mkurugenzi mtendaji TRL Shaban Kiko amesema treni hiyo yenye mabehewa 20
ambazo zina uwezo wa kubeba tani 40 kila behewa, imebeba mzigo wa
malighafi ya chuma ambao utasafirishwa kwa siku tatu hadi kuingia mkoani
kigoma na siku moja kuwasili mjini Bujumbura Burundi.
Kwa mujibu wa TRL imepunguza gharama za usafirishaji wa mizigo ya
kawaida na ile inayohifadhiwa katika makasha kwenda Burundi ambapo hivi
sasa inatoza kiasi cha dola 3,056 kwa behewa moja la mizigo ya kawaida
na dola 3024 kwa mizigo iliyofungwa kwenye makasha ikilinganishwa na
gharama zinazotozwa kwa njia ya barabara ambazo ni dola 3500.
No comments:
Write comments