JOSEPH Kasheku “Msukuma” Mbunge waa
Jimbo Geita Vijijini na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa
Geita ametoa siku tano za kuombwa na radhi na wanaodaiwa kuwa ni
maofisa usalama wa Taifa waliotoa taarifa za uongo dhidi yake na
kusababisha akamatwe Mjini Dodoma
Juzi Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma,
liliwatia nguvuni Msukuma, Hussein Bashe, Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini
na Adam Malima, aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mkuranga kwa madai ya
kupanga kufanya vurugu katika Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika jana.
Wanasiasa hao walikamatwa na kuhojiwa,
kabla ya kuachiwa kwa dhamana. Hata hivyo Msukuma amesema hawezi kukaa
kimya juu ya suala hilo na kwamba wapo maofisa usalama waliosambaza
taarifa juu yake na kusababisha hofu lazima wamuombe radhi.
“Hawa ni wapiga dili, Rais lazima
aiangalie upya Idara ya Usalama wa Taifa. Wameniundia mimi zengwe, mpaka
nikakamatwa, na nchi ikawa kwenye presha, kama chama kisipozungumza
mimi nitaenda kuzungumza na watoto wangu kama Askofu Gwajima
(Josephat),” amesema.
Mbunge huyo anayesifika kwa vituko
visivyoisha, amesema atapigania heshima yake kwani hajawahi kupata
kashfa na lazima atashinda.
“Sitazungumza kitaifa, nitaenda kuzungumza
na wapiga kura jimboni kwangu, nieleze kwanini watu wametengeneza
kinyago wakakiweka sebuleni halafu kinawatisha wenyewe. Kama kuna
usalama wa taifa aliyeshiriki natoa siku tano awe ameniomba msamaha,”
amesema Msukuma.
Hofu ya kuibuka kwa vurugu katika mkutano
mkuu wa CCM uliofanyika jana iliibuka baada ya juzi Halmashauri Kuu –
NEC ya chama hicho kuchukua uamuzi wa kuwafukuza viongozi mbalimbali
wanaodaiwa kuwa walikisaliti chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka
2015.
Waliofukuzwa uanachama ni pamoja na
wenyeviti wa CCM katika mikoa minne wakiwemo Ramadhani Madabida (Dar es
Salaam) na Jesca Msambatavangu (Iringa). Sophia Simba, Mwenyekiti wa
Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum
alikutana na kadhia hiyo
No comments:
Write comments