Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim
Lipumba amemshutumu Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad kwamba
anawatisha wajumbe wa ngazi mbalimbali za chama hicho.
“Kwa muda mrefu tangu Septemba 23, 2016
nimekuwa natoa wito kwa katibu mkuu aje ofisini Buguruni nimpe maelekezo
ya ujenzi wa chama chetu. Nimemuandikia memo na kumtumia barua pepe
lakini mpaka leo hajafika licha ya kuwa makazi yake yako Mtaa wa Sharif
Shamba, Wilaya ya Ilala jirani na ofisi kuu, Buguruni.
“Hivi sasa na mimi nimebaini wazi kuwa
katibu mkuu hana nia ya kujenga CUF imara Tanzania Bara. Vitendo vyake
ni mwendelezo wa imani na dhamira yake ya kuwapo kwa Muungano wa mkataba
kama alivyotoa maoni yake binafsi kwenye Tume ya Jaji Warioba,” amesema
Profesa Lipumba.
Mgogoro katika chama hicho ulishika kasi
mwishoni mwa mwaka jana baada ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
kumtambua Profesa Lipumba kama Mwenyekiti halali wa CUF, wakati
alishatangaza kujiuzulu nafasi yake kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 jambo
lililosababisha kukigawa katika makundi mawili
No comments:
Write comments