Mwanafunzi azidiwa na kukimbizwa hospitali baada ya mwalimu kumchapa viboko 10
Mwanafunzi
wa darasa la tatu katika shule ya msingi madeke halmashauri ya wilaya
ya njombe mwenye umri wa miaka 10 inadaiwa kuwa anaendelea kuugulia
maumivu ya adhabu ya kuchapwa viboko visivyopungua 10 na mwalimu wake wa
hesabu baada ya kufeli somo hilo hapo machi 21 mwaka huu
Kwa mujibu wa baba mzazi wa mtoto huyo
Bonface Manga Kwa masharti ya kutorekodiwa na waandishi mwanae Hosea
Manga alichapwa viboko kumi na mwalimu wake na kisha akazidiwa na
kukimbizwa hospitali.
Kutoka hospitali ya teule ya Mkoa wa
Njombe Kibena ambako mtoto huyo amelazwa hali yake bado ingali si nzuri
kwa kuwa hawezi kusimama wala kutembea licha ya kaimu mganga mfawidhi Wa
hospitali hiyo Isaya mvinge kueleza kuwa uchunguzi wa kitabibu bado
unaendelea
Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya
wilaya ya Njombe Kupitia Mkurugenzi Mtendaji monica kwiluvya anakiri
kupokea taarifa kwa njia ya simu kutoka kwa afisa elimu kata kuwa
mwalimu aliyehusika anashikiliwa na polisi
Jitihada za kupata taarifa ya jeshi la
polisi zimegonga mwamba baada a kamanda wa jeshi la polisi kueleza kuwa
yuko nje ya mkoa kikazi.
No comments:
Write comments