Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya
Kikwete leo amezindua Taasisi ya Maendeleo ya Jakaya Mrisho Kikwete
(JMKF).Taasisi hiyo imeundwa ili kusaidia Tanzania na Afrika katika
kuimarisha amani, afya, utawala bora na maendeleo endelevu.
Taasisi hiyo inajikita katika maendeleo
endelevu kwa kusaidiana na wadau wengine kukabiliana na umaskini,
kusaidia mkulima mdogo, kulinda mazingira na kukabiliana na athari za
tabia nchi. Baada ya uzinduzi huo Mbunge wa Kigoma Mjini
(ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amempongeza Rais huyo mstaafu kupitia
akaunti yake ya Facebook:
“Hongera Sana Rais Mstaafu Jakaya Mrisho
Kikwete kwa kuzindua Mfuko Wa Wakf Wa Jakaya Kikwete Foundation. Natumai
utaitumikia vema nchi yetu na bara la Afrika katika ustaafu wako. Jambo
moja kubwa uwekeze kwalo ni kuandaa Viongozi Vijana. Naona timu
imesheheni watu wenye uwezo mkubwa. Kila la kheri
No comments:
Write comments