Mratibu wa ushiriki wa Tanzania katika maonyesho hayo ambaye pia ni
Meneja Masoko wa Bodi ya TTB, Geofrey Meena amesema TTB imejipanga
vilivyo kuitangaza Tanzania kama eneo bora la utalii duniani ambapo
pamoja na kuendelea kuvitangaza vivutio v kama vile mlima Kilimanjaro,
Bonde la Ngorongoro, Hifadhi za Taifa, fukwe na maeneo mbalimbali ya
kihistoria.
Pia mwaka huu mkazo umewekwa katika kutangaza ushahidi wa nyayo za
binadamu wa kale (Zamadamu) uliovumbuliwa miaka milioni nne iliyopita
katika eneo la Laetoli lililoko takribani kilometa 45 kusini mwa Olduvai
Gorge.
“Pamoja na kuvumbuliwa kwa fuvu la anayesadikiwa kuwa ni binadamu wa
kwanza kabisa duniani huko Olduvai Gorge Ngorongoro, lakini katika
kuendelea kudhihirisha kuwa Binadamu wa kwanza aliishi Tanzania tumeamua
katika maonesho ya mwaka huu kuja na ushahidi unaoelezea ukweli huo
kwamba Binadamu asili yake ni Tanzania,” amesema Meena
Wednesday 8 March 2017
TTB yaitangaza Tanzania eneo bora la utalii duniani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Write comments