Wednesday 8 March 2017

Ubungo yatoa msaada hospitali ya Sinza Palestina

Halmashuri mpya ya Ubungo imetoa msaada wa vitu mbalimbali zikiwamo khanga na sabuni katika hospitali ya wilaya ya hiyo Sinza Palestina ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wanawake duniani.
Msaada wenye thamani ya zaidi ya Sh2 milioni umetolewa leo asubuhi na Meya wa Ubungo, Boniface Jacob akiambatana na maofisa wa wilaya hiyo.
Jacob amesema msaada huo ni jitahada mbalimbali za kuunga mkono siku wanawake kwa ni watu muhimu wa kuendesha gurudumu la maendeleo na kwamba halmashauri hiyo ipo katika kuboresha hospitali ya hiyo iwe ya kisasa.
Mmoja wa kinamama Ester William aliishukuru manispaa hiyo kwa kuwajali ikiwamo kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo na Mungu awabariki

No comments:
Write comments