Thursday 6 April 2017

Spika Ndugai amtaka Halima Mdee aripoti kamati ya maadili ya bunge

Spika wa Bunge la Jamuhuri Job Ndugai amemtaka Mbunge wa Kawe Halima Mdee kuripoti katika Kamati ya Maadili Kinga na Madaraka ya Bunge ili kujibu tuhuma za utovu wa nidhamu wakati uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki ukiendelea.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee
Spika wa Bunge la Jamuhuri Job Ndugai amemtaka Mbunge wa Kawe Halima Mdee kuripoti katika Kamati ya Maadili Kinga na Madaraka ya Bunge ili kujibu tuhuma za utovu wa nidhamu wakati uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki ukiendelea.

Spika Ndugai amesema hadi ifikapo kesho majira ya saa tano Mbunge huyo anatakiwa awe tayari ameripoti katika kamati hiyo.

Ndugai ametoa agizo hilo bungeni Mjini Dodoma baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu

No comments:
Write comments