Saturday, 20 May 2017

MABINGWA WAPYA WA EPL WASHINDWA HILI

Chelsea wameshatwaa ubingwa nchini Uingereza huku ligi bado haijaisha, Chelsea watamalizia ligi Jumapili ambapo watacheza dhidi ya Sunderland ambao wameshashuka daraja.
Lakini Chelsea wanaonekana ni kati ya vilabu ambavyo haviamini kuhusu vipaji vya vijana wadogo (teenagers) badala yake wamekuwa wakiwapa wachezaji wenye umri mkubwa nafasi zaidi.
Klabu ya Everton ndio klabu ambayo inaongoza kwa kuchezesha wachezaji ambao hawajafikisha umri wa miaka 20 kwani hadi sasa Everton wamewapa vijana hao dakika 6132 hadi sasa.
Everton wanaonekana wanaongoza kuwapa nafasi vijana chini ya 20 kwani katika msimu uliopita waliwapa wachezaji chininya miaka 20 dakika 11582 hadi mwisho wa msimu uliopita.
Jose Mourinho ambaye amekuwa akipondwa kuwa hawapi nafasi vijana lakini msimu huu hadi sasa amewapa vijana chini ya miaka 20 dakika 1924 za kucheza.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp naye amejitahidi tahidi kuwapa nafasi vijana chini ya umri wa miaka 20, kwani hadi sasa Klopp ameshawapa vijana hao dakika 256 za kucheza.
Lakini huwezi amini kuhusu Chelsea kwani hadi sasa ambapo ligi inaelekea kuisha huwezi amini Antonio Conte hajawahi kuchezesha kinda wa miaka chini ya 20 hata mchezo mmoja.
Hiyo ni ajabu kwani timu ya vijana ya Chelsea iliyoko chini ya Jody Morris inaonekana bora kwani msimu huu wameweza kuchukua ubingwa wa FA kwa mara ya nne mfululizo

No comments:
Write comments