Saturday, 20 May 2017

SIMBA KUIPIGA YANGA GOLI LA KISIGINO

 
Japokuwa wameukosa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, hesabu zikienda sawa basi Simba itachota fedha nyingi zaidi msimu huu kuliko Yanga iliyotwaa ubingwa wa ligi kuu leo.


Ligi imeisha huku Yanga wakiongoza wakiwa na pointi 68 sawa na wapinzani wao wa jadi Simba ila wakiwa mabingwa kwa tofauta ya magoli ya kufunga na kufungwa

Simba iliyomaliza nafasi ya pili itapata Sh milioni 40 kama kifuta jasho wakati Yanga itapata Sh milioni 81, lakini Simba itapata fedha nyingine Sh milioni 50 endapo itatwaa ubingwa wa Kombe la FA.

Wikiendi ijayo Simba itacheza fainali ya Kombe la FA dhidi ya Mbao FC kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma na ikishinda itapata Sh milioni 50 ambapo jumla msimu huu itapata Sh milioni 90.

Hii ina maana kwamba, Yanga waliotwaa uchampioni msimu huu watapata  Sh milioni 81 pekee za zawadi ya ubingwa wakati Simba itapata Sh milioni 90, ikiizidi Yanga Sh milioni tisa.
kwa kutwaa ubingwa msimu huu Yanga wanakua wamefanikiwa kutwaa kwa mara ya 27 na mara ya 3 mfululizo chini ya nahodha wake Nadir Haroub

No comments:
Write comments