KARATASI HIZO IKIWEMO LISITI YA TRA ZINAONYESHA TAYARI SIMBA WAMEISHATUMA MALALAMIKO YAO FIFA. |
Ushahidi kuwa klabu ya Simba imewasilisha malalamiko yake kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), umepatikana.
Kitendo
cha Simba kuwasilisha rufaa hiyo na picha ikionyesha ushahidi huo,
inaonekana kuwakwaza zaidi ya mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wameanza
sherehe za ubingwa.
Baadhi ya mashabiki wa Yanga, wameonekana kukerwa na jambo hilo huku wakiwaita Simba “Wazee wa pointi za mezani”.
Lakini mashabiki wa Simba wamekuwa wakijibu mapigo na kusema, “Haki ni haki” na sheria itafuata mkondo wake.
Yanga na Simba zimemaliza ligi zikiwa na pointi 68 kila moja, lakini Yanga ina wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa GD.
Silaha
ya Simba, inabaki kuwa suala la pointi za Kagera na kama kweli Fifa
itaamuru irejeshewe, basi itafikisha pointi 71 na kutangazwa kuwa
bingwa.
Simba
ilishinda rufaa yake kupitia kamati ya Saa 72 ambayo ilibaini kuwa
kweli beki Mohammed Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano wakati Simba
ilipolala kwa mabao 2-1 katika mechi ya ligi Kuu Bara.
Lakini
Kagera Sugar ilikata rufaa katika kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za
Wachezaji na kushinda ikarejeshewa pointi zake tatu.
Hata
hivyo, wakati wa kutangaza kamati hiyo ya Katiba, Sheria na Hadhi za
Wachezaji haikutoa ufafanuzi wowote kuhusiana na Fakhi kama alikuwa na
kadi mbili au tatu za njano.
Badala yake ikasema rufaa ya Simba ilichelewa pia haikulipiwa hivyo kuifanya iwe batili.
Lakini
kuhusiana na pointi hizo tatu, inaonekana hata kama Simba isingekata
rufaa na kama kweli Fakhi ana kadi tatu za njano, basi automaticaly,
Kagera Sugar wangepokwa ushindi.
Hivyo,
Simba imeamua kwenda Fifa kuhakikisha inapata pointi tatu ambazo kama
itafanikiwa, basi moja kwa moja inatangazwa kuwa bingwa.
No comments:
Write comments