Fundi
mbao, Japhet Lendiman (38) mkazi wa Daraja Mbili, anashikiliwa na Jeshi
la Polisi, baada ya kubaka watoto wake wa kike wa darasa la sita na
kidato cha kwanza.
Akizungumzia
tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema
kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kiini cha tatizo hilo
ni nini na kufuatiwa na hatua ya kufikishwa mahakamani. Mtuhumiwa huyo
anashikiliwa na Jeshi la polisi tangu Juni 6, mwaka huu na upelelezi
unaendelea kubaini undani wa tukio hilo.
Akimzungumzia
mtuhumiwa huyo, mmoja wa majirani wa eneo hilo la Daraja Mbili (jina
limehifadhiwa) alidai kuwa mzazi huyo amezoeleka kwa tabia hiyo mbaya
mtaani kwao.
Alidai
kuwa mtuhumiwa huyo amezoea kubaka watoto wake mara kwa mara wakati
mama yao akiwa kazini na kwamba Mei 28 majira ya saa 9:00 alasiri
alimbaka tena mtoto wake (Jina tumelihifadhi) wa darasa la sita shule ya
Msingi Daraja Mbili ndipo taarifa zilipoanza kuzagaa mtaani.
“Siku
hiyo ya tukio lililosababisha mzazi huyo kukamatwa mtoto aliona sasa
uvumilivu umefika mwisho, alikwenda kwa mama mkubwa na kutoa taarifa
jinsi baba yake anavyomwingilia na kueleza kuwa anataka kunywa sumu ili
afe,” alieleza jirani huyo.
Alisema
baada ya maelezo hayo mama mkubwa aliamua kuhoji watoto wote wa shemeji
yake akiwemo mwingine wa umri wa miaka 14 (jina limeifadhiwa) ambaye
yupo kidato cha Kwanza Sekondari ya Felix Mrema, alikiri kuingiliwa na
baba yake tangu mwaka 2016.
No comments:
Write comments