Jeshi
la Polisi mkoa wa Kipolisi wa Moshi limezuia utaratibu wa kutoa
heshima za mwisho kwa kuutembeza katika barabara za viunga vya manispaa
hiyo, mwili aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema, Kilimanjaro, marehemu
Philemon Ndesamburo .
Majibu
ya barua yaliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Polisi Moshi, yamezuia mwili
huo kupitishwa katika barabara za kati kati ya mji kwa kile walichoeleza
kuwa leo Juni 5 na siku ya kazi na kuna shughuli za mbalimbali
zinazoendelea.
Sababu
ya pili iliyotolewa na ofisi hiyo ni kwamba wakiupitisha mwili huo
barabarani watasababisha msongamano mkubwa ambao utakuwa chanzo cha
usumbufu kwa watumiaji wengi wa barabarani.
“Ofisi
ya Mkuu wa polisi wa wilaya inatoa maelekezo kuwa mwili wa Ndesamburo
ukitolewa KCMC, upitishwe barabara ya YMCA kupitia Lucy Lameck Road hadi
uwanja wa michezo wa Majengo ambapo kumepangwa kufanyika kwa shughuli
zote za kutoa heshima za mwisho.
Jana
mmoja wa wanakamati ya mazishi ya Ndesamburo, Anthony Komu alisema
kuwa mwili wa Ndesamburo utachukuliwa KCMC saa 4 asubuhi na kupitishwa
katika barabara kuu za mji wa Moshi ili kuwawezesha ambao hawatapata
nafasi ya kufika Majengo, kuuaga mwili huo.
No comments:
Write comments